Posts

Featured Post

Sergio Ramos alivyozuia rekodi ya Real Madrid isivunjwe na FC Barcelona Dec 3 2016

Image
Baada ya presha na ubishi wa zaidi ya wiki moja wa mashabiki wa FC Barcelona na Real Madrid za Hispania, kubishana timu ipi itapata ushindi katika mchezo wa El Clasico uliochezwa katika uwanja wa Nou Camp jijini Barcelona, hatimae ubishi umemalizwa usiku wa December 3 2016. Timu za Barcelona na Real Madrid zote ziliingia zikiwa na kumbukumbu kuwa mchezo wao wa mara ya mwisho kumalizika pasipo goli ilikuwa ni mwaka 2002, huku Real Madrid waliingia kutetea rekodi yao ya kucheza mechi yao ya 33 bila kuruhusu kupoteza mchezo hata mmoja na kutoka sare mechi 6 pekee. December 3 2016 katika uwanja wa Nou Camp mchezo huo wa El Clasico umemalizika kwa sare ya kufungana goli 1-1, FC Barcelona ndio walikuwa wa kwanza kupata goli dakika ya 53 kupitia kwa Luis Suarez na Real Madrid wakafanikiwa kusawazisha goli dakika ya 90 kupitia kwa Sergio Ramos. Msimamo wa ligi baada ya mechi hiyo